Nenda kwa yaliyomo

Lillian Nakate

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Lillian Nakate Segujja (11 Agosti 1978) ni mhandisi na mwanasiasa wa nchini Uganda. Yeye ni Mbunge wa kike aliyewakilisha jimbo la Luweero katika Bunge la 10 mnamo (2016 hadi 2021) nchini Uganda.[1]

Alizaliwa huko Wobulenzi, wilaya ya luweero, mkoa wa kati wa Uganda, mnamo 11 Agosti 1978.[1] Wazazi wake ni marehemu Francis Segujja na Annet Segujja.[2] Lilian alisoma katika shule ya msingi ya wobulenzi. Alisoma katika shule mbalimbali za sekondari ikiwa ni pamoja na shule ya sekondari ya saint john huko nandere, wilaya ya luweero, shule ya sekondari ya mulusa academy, huko wobulenzi, na kumalizia elimu yake ya sekondari katika shule ya sekondari ya Luteete huko bamunanika. Baadae alirudi katika shule ya mulusa academy kuendelea na elimu yake ya kidato cha tano na cha sita.[1][2]

Alijiunga na Chuo Kikuu cha Ufundi cha Kyambogo Uganda Polytechnic na alisoma diploma ya usanifu wa Majengo, na kuhitimu mnamo mwaka 2000. Mwaka 2007 alimaliza masomo yake katika chuo kikuu cha makerere, chuo kikuu kikubwa zaidi cha umma nchini Uganda, akitunukiwa shahada ya sayansi (BSc) katika uhandisi wa Majengo. Lillian baadae aliendelea na masomo yake na kusoma shahada ya umahiri mnamo mwaka 2011 katika chuo kikuu cha makerere. Pia alitunukiwa cheti katika mradi wa mipango na Usimamizi.

Pia alitunukiwa tuzo na taasisi ya takwimu na biashara katika chuo kikuu cha makerere mwaka 2008. shahada yake ya fedha na usimamizi wa biashara na ujenzi wa barabara ilitolewa mwaka 2013, na taasisi ya biashara ya multitech huko Kampala, mji mkuu wa Uganda.[1][2]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 POUG (1 Desemba 2017). "Parliament of Uganda: Members of The 10th Parliament: Nakate Segujja Lillian". Kampala: Parliament of Uganda (POUG). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-03-21. Iliwekwa mnamo 1 Desemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 Baike, Prisca (13 Aprili 2017). "Politics Has Taught Lillian Nakate Calmness". The Observer (Uganda) via AllAfrica.com. Kampala. Iliwekwa mnamo 1 Desemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lillian Nakate kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.