Kondoa-Irangi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Kondoa-Irangi ni jina la kihistoria kwa ajili ya mmojawapo kati ya mikoa ya kiutawala katika koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (leo hii: Tanzania, Rwanda na Burundi).

Eneo la mkoa huo ulikuwa na kilomita za mraba 55,600.

Makao makuu ya mkoa huo yalikuwa Kondoa Mjini. Ofisi ndogo ya mkoa ilikuwepo Mkalama.

Historia ya Mkoa wa Kondoa-Irangi[hariri | hariri chanzo]

Mkoa huo ulianzishwa mwaka 1912 kutokana na maeneo ya mkoa wa Kilimatinde uliomegwa wakati ule.

Wakati wa utawala wa Uingereza juu ya Tanganyika mkoa huu wa Kondoa-Irangi uliendelezwa hadi kuingizwa baadaye katika jimbo la kati (Central Province).

Wakazi na ufugaji[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1913 kulikuwa na wakazi Waafrika 218,300 na Wazungu 70.

Waafrika walifuga wakati ule ng'ombe 196,370, kondoo 172,010, mbuzi 150,830 na punda 5,650.

Walowezi Wazungu walikuwa na kaya 10 zenye eneo la kilomita za mraba 30.3 wakifuga ng'ombe 2,366, mbuzi na kondoo 402, nguruwe 282, punda 257 na mbuni 28.

Vita Kuu ya Kwanza[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia kulikuwa hapa na mapigano makubwa kati ya majeshi ya Uingereza na jeshi la Kijerumani la Schutztruppe.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]