Kima (mnyama)
Kima | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kima buluu
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Oda ndogo 2:
|
Kima ni mamalia yeyote wa hali ya juu katika familia ya juu Cercopithecoidea (kima wa Dunia ya Kale) na oda ndogo Platyrrhini (Kima wa Dunia Mpya), kwa hivyo kima wa juu wasio Prosimii (nusuoda ya zamani) au masokwe na nyani. Kuna takriban spishi 264 wanaofahamika wa kima wanaowakilisha kundi kubwa la mamalia wa hali ya juu. Kima huonwa kama ni mwenye akili sana na tofauti na masokwe; kima daima huwa na mkia. Kima wa Dunia ya Kale wanafanana zaidi na masokwe kuliko kima wa Dunia Mpya.
Tabia
[hariri | hariri chanzo]Kima wana ukubwa tofauti kutoka milimita za urefu 140 – 160 (pamoja na mkia) na uzito wa gramu 120 mpaka 140, mpaka urefu wa mita moja wa kilo 35. Wachache huishi kwenye miti wakati mwingine huishi kwenye savana. Chakula chao ni matunda, majani, mbegu, maua, mayai na wanyama wadogo (ikijumuishwa wadudu na buibui).
Kima wote wa Dunia Mpya wana mikia tofauti na wa Dunia ya Kale. Baadhi ya kima wana uoni wa rangi na wengine hawana. Huku kima wa Dunia Mpya wakiwa na macho kwa mbele walionekana tofauti hata baina yao hasa pua, mashavu na sehemu ya nyuma kwa ujumla.
Uainishaji
[hariri | hariri chanzo]Ifuatayo ni orodha ikionesha familia za kima.
- ODA PRIMATES
- Nusuoda Strepsirrhini: komba, koni na lemuri
- Nusuoda Haplorrhini
- Oda ya chini Tarsiiformes
- Familia Tarsiidae: komba vidole-virefu
- Oda ya chini Simiiformes: kima
- Oda ndogo Platyrrhini: kima wa Dunia Mpya
- Familia Cebidae
- Familia Aotidae
- Familia Pitheciidae
- Familia Atelidae
- Oda ndogo Catarrhini: kima wa Dunia ya Kale
- Familia ya juu Cercopithecoidea
- Familia ya juu Hominoidea
- Familia Hylobatidae: masokwe wadogo
- Familia Hominidae: masokwe wakubwa na binadamu
- Oda ndogo Platyrrhini: kima wa Dunia Mpya
- Oda ya chini Tarsiiformes
Mahusiano na binadamu
[hariri | hariri chanzo]Spishi tofauti za kima wana mahusiano na binadamu, baadhi yao hufugwa kama wanyama wa nyumbani na hutumika kama kifani cha binadamu kwenye maabara na safari ya angani. Pia huwahudumia binadamu wenye udhaifu. Kuna baadhi ya kima huonekana kama wanyama waharibifu wa mazao.[1] Kima ambao pia wapo kwenye mbuga ya watalii lakini hugeuka kama kitishio kwa watalii huona kama kuna kikwazo kwa binadamu hivyo tatizo dogo.
Kwenye dini huwakilisha werevu.
Kama huduma kwa watu wasiojiweza
[hariri | hariri chanzo]Baadhi ya mashirika yamekuwa yakiwafunza kima wa wakapuchini kama wasaidizi kuwasaidia watu wenye matatizo ya uti wa mgongo na matatizo mengine ya kutembea. Baada ya mafunzo kutosha kima hawa huweza kuwahudumia barabara walemavu wakiwa ndani ya nyumba, kima husaidia kupika, kuosha uso na kufungua chupa za vinywaji.
Kwenye tafiti
[hariri | hariri chanzo]Kima aina ya Macaques wale wa Afrika Green Monkeys, hutumika kwenye tafiti nyingi aidha kwa kukamatwa porini au kulazimishwa. Hutumika sana kutokana na uwezo wao mkubwa wa kubeba vitu, kuzaliana kwa muda mfupi na kufanana kwao sana kisaikolojia na kimaumbile na binadamu.
Angani
[hariri | hariri chanzo]Nchi nyingi zinawatumia kima kama sehemu yao ya tafiti za anga kujumuisha Marekani na Ufaransa. Kima wa kwanza kwenda angani aliitwa Albert II, ambaye aliruka angani na roketi ya Marekani, mnamo Juni 14, 1949.
Kama chakula
[hariri | hariri chanzo]Ubongo wa kima unaliwa kama chakula kitamu huko Asia ya Kusini, China na Afrika.[2] Kwa taratibu ya dini ya kiislamu kula nyani ni marufuku kabisa. Hata hivyo kima huliwa sehemu nyingine za Afrika, ambako nyama yake huuzwa kama nyama ya msituni.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑
This citation will be automatically completed in the next few minutes. You can jump the queue or expand by hand - ↑ Bonné, J. (2005-10-28). "Some bravery as a side dish". msnbc.com. Iliwekwa mnamo 2009-08-15.
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.