Kiliani wa Wurzburg

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Mt. Kiliani.

Kiliani wa Wurzburg (Cloughballybeg, karibu na Mullagh, County Cavan, Ireland, 644 hivi - Wurzburg, leo nchini Ujerumani, 8 Julai 689) alikuwa mmonaki, halafu kwa kibali cha Papa Kononi[1] askofu mmisionari katika Frankonia, kaskazini mwa Bavaria ya leo, kuanzia mwaka 686 hadi alipofia dini yake, labda pamoja na wenzake 4.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini[2].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 8 Julai[3].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.