Nenda kwa yaliyomo

Kevin-Prince Boateng

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kevin-Prince Boateng.
Boateng akiichezea Ghana katika kombe la dunia 2010.

Kevin-Prince Boateng (hutamkwa [ˈkɛvɪn pʁɪns bo.aˈtɛŋ]; amezaliwa 6 Machi 1987 na wazazi wa mataifa tofauti: baba Mghana mama Mjerumani. Ni bingwa wa mpira wa miguu ambaye kwa sasa anachezea timu ya Eintracht Frankfurt.

Ni kiungo ambaye anaweza kucheza kama mshambuliaji. Boateng inajulikana kwa nguvu zake, kasi anapokuwa na mpira, vyenga vya kushangaza. Tovuti rasmi ya FIFA alieleza Boateng kama "mchezaji aliyebarikiwa kuwa na nguvu, kasi, hatari katika kufunga mabao.

Boateng alianza kazi yake katika klabu ya Reinickendorfer Füchse mwanzoni mwa mwaka 1994 akiwa na miaka sita kabla ya kujiunga na Hertha BSC 1 Julai 1994 akiwa na umri wa miaka saba.

Baada ya kujitokeza kutoka timu ya Hertha, Boateng alicheza Hertha BSC II kwa misimu miwili akapandishwa kikosi cha timu ya kwanza ya Hertha katika msimu wa 2005-06.

Boateng alicheza Portsmouth katika kombe la FA mwishoni mwa mwaka 2010 katika ligi kuu ya Uingereza, klabu ya Portsmouth ilimsainisha Boateng kwa mkataba wa miaka mitatu mwaka 2009 kwa ada ya kuripotiwa ya £ milioni 4. Tarehe 12 Septemba 2009, alifunga bao lake la kwanza dhidi ya Chelsea F.C., na alikuwa mchezaji bora wa mwezi Agosti katika mwaka huo. Alimaliza msimu akiwa na mabao matatu katika michezo 22.

Mwezi Mei mwaka 2010, Portsmouth alicheza na Chelsea katika kombe la FA, ambapo Chelsea ilishinda 1-0. Wakati wa mechi, Boateng alimchezea rafu kiungo wa Chelsea Michael Ballack, na kumjeruhi kiwiko. Boateng alidai kwamba Ballack alimpiga katika uso kabla ya yeye kumchezea rafu, na alimuomba msamaaha Ballack kwa rafu aliyomchezea.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kevin-Prince Boateng kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.