Keremoni na wenzake

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Keremoni na wenzake (walifariki katikati ya karne ya 3) walikuwa Wakristo wa Misri waliokimbia dhuluma ya kaisari Decius dhidi yao.

Dionisi wa Aleksandria, katika barua kwa Fabio wa Antiokia [1] iliyoripotiwa na Eusebi wa Kaisarea pia [2], alishuhudia ushujaa wa wafiadini na kusikitikia kifo cha wengi walipokimbilia jangwani au milimani, kati yao askofu mzee Keremoni wa Nilopoli na mke wake[3].

Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 22 Desemba[4].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. PG, X, 1306
  2. Hist. Eccl., VI, 41, katika PG, XX, 605-12
  3. Eusebio, VI, 42, PG, XX, 614
  4. https://catholicsaints.info/saint-chaeremon-of-nilopolis/
Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Keremoni na wenzake kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.