Julian Draxler

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Julian Draxler kushoto mwa Mesut Ozil baada ya Ujerumani kushinda kombe la dunia 2014.

Julian Draxler (matamshi ya Kijerumani: [juːli̯aːn dʁakslɐ]; alizaliwa Septemba 20, 1993) ni mchezaji wa soka wa Ujerumani ambaye anacheza kama winga wa klabu ya Ufaransa Paris Saint-Germain (PSG) na timu ya taifa ya Ujerumani. Anajulikana kwa uwezo wake wa kutumia miguu yote, kasi yake, na nguvu za kupiga mashuti makali.

Draxler alianza kucheza Bundesliga na timu yake ya kwanza Schalke 04 akiwa na umri wa miaka 17 mnamo Januari 2011.

Kwa jumla, alicheza mechi 171 na Schalke 04, alifunga mabao 64, kabla ya kuhamia VfL Wolfsburg mwaka 2015.

Mnamo Januari 2017, alijiunga na PSG.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Julian Draxler kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.