Nenda kwa yaliyomo

Joji, Aureli na wenzao

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Joji, Aureli na wenzao Natalia (jina la awali: Sabigoto), Felisi na Liliosa (walifariki Cordoba, leo nchini Hispania, 852) walikuwa Wakristo waliokatwa kichwa na Abd ar-Rahman II, Emir wa Cordoba, chini ya utawala wa Waislamu. Wao ni miongoni mwa Mashahidi wa Córdoba, Wakristo 48 waliouawa katika jiji hilo kati ya miaka 850 na 859.

Joji alikuwa shemasi mmonaki kutoka Syria-Palestina. Wenzake walikuwa watu wa ndoa wenyeji[1].

Wakitamani kushuhudia imani yao kwa kufia dini, walipotupwa gerezani hawakuacha kumuimbia sifa Kristo.

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 27 Julai [2].

Maisha ya Aureli na Natalia

[hariri | hariri chanzo]

Aureli alizaliwa katika familia tajiri huko Seville. Baba yake alikuwa Mwarabu Mwislamu na mama yake Mkristo kutoka Uhispania. Akiwa yatima alipokuwa mtoto, alilelewa na shangazi, ambaye inaelekea alikuwa Mkristo kwa siri. Wakati huo, Wakristo waliteswa katika falme za Wamoor za Hispania.[3].

Aureli alimuoa Sabigoto, msichana kutoka familia ya Kiislamu. Baada ya harusi, Sabigoto aliamua kubadili dini na kuwa Mkristo na kuchukua jina la Natalia. Wenzi hao waliishi Emirate ya Córdoba, walikuwa na binti, na waliishi kwa siri kama Wakristo. Wakati huo, kubadili dini kutoka Uislamu hadi Ukristo ilikuwa ni hatia yenye adhabu ya kifo.[4].

Siku moja, Aureli aliona kupigwa viboko hadharani kwa mfanyabiashara Mkristo ambaye alikuwa amekiri hadharani imani yake katika Kristo. Wakiwa wameshtushwa na tukio hili, Aureli na Natalia waliamua kwamba hawawezi tena kuficha imani yao. Walitenga pesa kwa ajili ya binti yao na kuwagawia maskini akiba iliyobaki. Kisha wakaanza kutangaza waziwazi imani yao na kuwatunza Wakristo waliokuwa gerezani.

Masalia ya Aureli yanatunzwa katika madhabahu katika Basilica ya Metropolitan Cathedral ya Santa María la Antigua huko Mji wa Panama[5].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Marejeo ya Kiswahili

[hariri | hariri chanzo]
  • John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 257
  • Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 216

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.