Johnny Tri Nguyen

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Johnny Tri Nguyen
Johnny Tri Nguyen.
Johnny Tri Nguyen.
Jina la kuzaliwa Johnny Tri Nguyen
Alizaliwa 16 Februari 1974
Vietnam
Mahusiano Ngo Thanh Van

Johnny Tri Nguyen (Kivietnamese: Nguyễn Chánh Minh Trí, amezaliwa tar. 16 Februari 1974 katika mkoa wa Binh Duong, Vietnam ya Kusini) ni mwigizaji wa filamu, tamthilia, "stunt" na vilevile ni "martial artist" wa Kivietnam-Kimarekani.

Maisha ya awali kwa ufupi[hariri | hariri chanzo]

Johnny aliondoka nchini Vietnam akiwa na umri wa miaka 8 akiwa pamoja na familia yake, mama, baba, kaka yake, na dada yake wote wakaelekea zao mjini Los Angeles. Johnny ni nusu Mchina na nusu Mvietnam, mama yake ni Mchina.

Familia na filamu[hariri | hariri chanzo]

Johnny Nguyen ametoka katika familia yenye asili ya uigizaji. Mjomba wake ni Bw. Nguyen Chanh Tin, mwigizaji filamu wa zamani wa Kivietnam, wakati kaka yake Bw. Charlie Nguyen, ambaye amewahi kuongoza filamu nyingi maarufu za kampuni ya Van Son Entertainment videos.

Shughuri za filamu kwa ufupi[hariri | hariri chanzo]

Filamu alizocheza Johnny ni kama vile Tom-Yum-Goong (ya Tony Jaa) na Cradle 2 the Grave. Kazi za ustant kacheza katika filamu ya Spider-Man sehemu ya pili na alicheza kama Green Goblin katika sehemu za mwanzo-mwanzo. Johnny ni mtaalmu wa kupambana kwa kung fu, wushu, tai chi, aikido, na vovinam.

Filamu alizoigiza[hariri | hariri chanzo]

Filamu alizocheza kama mwigizaji[hariri | hariri chanzo]

 • Nu Hon Than Chet (2008)
 • Saigon Eclipse (2007)
 • The Rebel (2006)
 • Adventures of Johnny Tao: Rock Around the Dragon (2006)
 • Hon Truong Ba Da Hang Thit (2006)
 • House of the Dead 2: Dead Aim (2005)
 • Tom-Yum-Goong (2005, released as The Protector in 2006)
 • Demon Hunter (2005)
 • House of the Dead 2: Dead Aim (2005)
 • Color Blind (2005)
 • Sledge: The Untold Story (2005)
 • Max Havoc: Curse of the Dragon (2004)
 • First Morning (2004)
 • Ella Enchanted (2004)
 • XMA (2004)
 • The Shield (2004)
 • Alias (2003)
 • Cradle 2 the Grave (2003)
 • The Master of Disguise (2002)
 • Martial Law (1998)

Filamu alizocheza kama stant(stant ni mtu anaeigiza katika sehemu za hatari)[hariri | hariri chanzo]

 • The Perfect Sleep (2005)
 • Jarhead (2005)
 • Serenity (2005)
 • Color Blind (2005)
 • Ella Enchanted (2004)
 • Spider-Man 2 (2004)
 • Collateral (2004)
 • Starship Troopers 2 (2004)
 • Nudity Required (2002)
 • Spider-Man (2002)
 • We Were Soldiers (2002)
 • Angel (1999)
 • Charmed (1998)
 • Mortal Kombat: Conquest (1998)
 • Buffy the Vampire Slayer (1997)

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Akizungumzia kabila lake kwenye mahojiano na Tom-Yum-Go (WMV file))

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]