Nenda kwa yaliyomo

Issyk Kul

Majiranukta: 42°25′N 77°15′E / 42.417°N 77.250°E / 42.417; 77.250
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ziwa Issyk Kul
Issyk Kul katikati ya milima ynye theluji; picha ya satelaiti
Issyk Kul katikati ya milima ynye theluji; picha ya satelaiti
Mahali 42°25′N 77°15′E / 42.417°N 77.250°E / 42.417; 77.250
Nchi zinazopakana Kirgizia
Eneo la maji km2 6,236
Kina cha chini m 668
Mito inayoingia (maji ya barafuto)
Mito inayotoka (uvukuzaji)
Kimo cha uso wa maji
juu ya UB
m 1,607
Miji mikubwa ufukoni Cholpon-Ata, Karakol

Issyk Kul (kwa Kikirgizi: Yssykköl "ziwa moto"; kwa Kirusi: Иссык-Куль) ni ziwa kubwa zaidi la nchi ya Kirgizia katika Asia ya Kati.

Ziwa hilo liko katika milima ya Tian Shan na uso wake upo mita 1,607 juu ya usawa wa bahari. Eneo la maji ni km2 6236 na hivyo ni ziwa la mlimani kubwa la pili duniani baada ya Ziwa Titicaca (Amerika Kusini). Mito 118 inapeleka maji yao katika Issyk Kul. Muhimu zaidi ni mito ya Jergalan, Tjup, Dschuku, Karakol na Jeti-Ogus.

Tabia za pekee

[hariri | hariri chanzo]

Maji ya Yssyk Kul hayagandi wakati wa baridi ingawa halijoto ya hewa hupoa hadi sentigredi 20 chini ya sifuri. Inaaminiwa sababu yake hasa ni mwendo wa kuchanganya maji ya chini (yenye halijoto ya °C 4) na maji ya usoni (yanayopoa zaidi wakati wa baridi). Sababu ya ziada ni kiasi kidogo cha chumvi katika maji ya ziwa kinachofikia asilimia 0.6 (maji ya bahari huwa na % 3.5)

Ziwa hilo halina njia ya kutoka, kwa hiyo maji yote yanayoingia hulingana na kiasi kinachopotea tena kwa njia ya uvukizaji.

Riwaya kadhaa za mwandishi Genghis Aitmatov zinasimulia hadithi za Issyk Kul.

Matumizi

[hariri | hariri chanzo]

Zamani Issyk Kul ilikuwa na maana kwa uvuvi wa samaki; siku hizi hutumiwa zaidi kwa utalii. Karibu na ziwa iko miji ya Karakol na Cholpon-Ata.

Wakati wa Umoja wa Kisovyeti (hadi mwaka 1991) maeneo makubwa ya ziwa na mwambao yalikuwa maeneo ya kijeshi; wanamaji walifanya hapa utafiti na majaribio ya topido.


Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Issyk Kul kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.