Irenarki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Irenarki (alifariki Sebaste katika Armenia Ndogo, leo Sivas, Uturuki, 303 hivi) alikuwa askari ambaye aliongokea Ukristo kwa kuona ushujaa wa wanawake wa dini hiyo katika kukabili kifodini kwa ajili ya imani yao.

Hatimaye yeye naye aliuawa kwa shoka katika dhuluma ya kaisari Dioklesyano[1].

Ndiyo sababu anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Novemba[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.