Irène Joliot-Curie
Mandhari
Irène Joliet-Curie (12 Septemba 1897 - 17 Machi 1956) alikuwa mwanasayansi wa Ufaransa.
Alishinda tuzo ya Nobel kwa Kemia mwaka wa 1935 pamoja na mumewe, Frédéric Joliot. Curie alikuwa binti Pierre Curie na Marie Curie
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Curie alianza masomo yake katika kitivo cha Sayansi huko Paris. Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza (1914-1918), aliwahi kuwa mbobeaji kwenye mambo ya eksirei.
Wakati wa Vita Kuu ya kwanza ya Dunia, alimsaidia mama yake kutumia teknolojia ya eksirei katika hospitali za kijeshi. Aliwasaidia wafanyakazi wa mionzi.
Curie kisha alihitimu kutoka Sorbonne huko Paris akawa Daktari wa Sayansi mwaka wa 1925. Alifanya tasnifu yake juu ya mnururisho α wa poloniamu akapata shahada ya kufanya kazi kwenye mambo ya mionzi katika poloniamu.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Irène Joliot-Curie kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |