Ipelele
Kata ya Ipelele | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Njombe |
Wilaya | Makete |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 5,933 |
Ipelele ni kata ya Wilaya ya Makete katika Mkoa wa Njombe, Tanzania. Msimbo wa posta ni 59520.
Ni eneo dogo sana lenye vijiji sita yaani Ubiluko, Ipelele, Makwaranga, Mbanga, Makeve na Missiwa.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 5,933 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 4,890 [2] walioishi humo. Kata hiyo ina kabila dogo liitwalo Wamagoma.
Wenyeji wa eneo hilo wanajishughulisha na kilimo cha mahindi, ngano, njegere na viazi. Hata hivyo inasemekana walikuwa wafugaji wa ng'ombe wakubwa katika milima ya Ikata na Magoma; mpaka sasa ufugaji upo ila si sawa na zamani.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.nbs.go.tz, uk 211
- ↑ "Sensa ya 2012, Njombe - Makete DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2021-01-16.
Kata za Wilaya ya Makete - Tanzania | ||
---|---|---|
Bulongwa | Ikuwo | Iniho | Ipelele | Ipepo | Isapulano | Itundu | Iwawa | Kigala | Kigulu | Kinyika | Kipagalo | Kitulo | Lupalilo | Lupila | Luwumbu | Mang'oto | Matamba | Mbalatse | Mfumbi | Mlondwe | Tandala | Ukwama |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Njombe bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ipelele kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |