Mang'oto
Mang`oto ni jina la kata ya Wilaya ya Makete katika Mkoa wa Njombe, Tanzania. Wakati wa wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 3,781 [1] walioishi humo. Msimbo wa posta ni 59502
Kata ina vijiji sita: Mang'oto, Malembuli, Makangalawe,Usungilo, Ilindiwe, na Ibaga. Katika historia ya uongozi wa kata, kabla kidogo na baada ya vijiji vya Ujamaaa kiongozi (mwenyekiti) wa kata alikuwa ndugu Lonati Mwapangile Sanga.
Wakazi wa kati hii hulima zaidi ngano, mahindi na numbu pamoja na mbogamboga pia kata hii ni maarufu kwa kilimo cha shayiri katika vijiji vya Makangalawe na Ibaga pia wakazi hawa hupanada miti kwa ajili ya kujipatia fedha
Pia kata hii ina jumla ya shule 6 za msingi na 1 ya sekondari pia ina zahanati 3 wakazi hawa pia huweza kutumia tiba za asili kama wakunga wa jadi walipo maeneo hayo
Ibwela ni sehemu ya soko katika kata ya Mang'oto. Sehemu hii ndipo wakazi wengi wanapopatikana ni nje kidogo toka stendi ya kata. Bidhaa za kila aina hupatikana hapo.
Marejeo
- ↑ Sensa ya 2012, Njombe - Makete DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2017-03-29.
![]() |
Kata za Wilaya ya Makete - Tanzania | ![]() |
---|---|---|
Bulongwa | Ikuwo | Iniho | Ipelele | Ipepo | Isapulano | Itundu | Iwawa | Kigala | Kigulu | Kinyika | Kipagalo | Kitulo | Lupalilo | Lupila | Luwumbu | Mang'oto | Matamba | Mbalatse | Mfumbi | Mlondwe | Tandala | Ukwama |
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Njombe bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mang'oto kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |