Nenda kwa yaliyomo

Igeleke

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Igeleke ni mtaa uliopo katika kata ya Kambarage, wilaya ya Njombe, mkoa wa Njombe.

Wakazi wake kwa asilimia kubwa ni Wabena na kwa uchache makabila mengine kama vile Wakinga, Wahehe, Wawanji pamoja na makabila kutoka mikoa mbalimbali kote nchini Tanzania.

Wakazi wake wanajishughulisha na shughuli mbalimbali zikiwemo za Biashara kama vile mbao, kokoto na mazao, kilimo cha Viazi Mbatata na Viazi Vitamu, Mahindi, Njegere, maharage na uvunjaji wa mawe (kokoto) katika mwamba mkubwa wa matalawe (Ganga lya ndefu).

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Njombe bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Igeleke kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.