Ibn Sina

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Ibn Sina (pia: Avicenna) aliyeitwa kwa jina kamili Abū ʿAlī al-Ḥusayn ibn ʿAbd Allāh ibn Sīnā (Kar. ابو علی الحسین ابن عبدالله ابن سینا) ni kati ya wataalamu na wanafalsafa mashuhuri kabisa katika historia ya Uislamu.

Alizaliwa mnamo mwaka 980 karibu na mji wa Bukhara [1][2] katika Khorasan akafa mwaka 1037 mjini Hamadan [3][4]) katika Uajemi.

Alishughulika sayansi nyingi alikuwa mtabibu na pia mtaalamu wa fizikia, sheria, hisabati, astronomia na kemia.

Kwa jumla alitoa maandiko 450 kuhusu maada mbalimbali na 240 kati haya zimepatikana hadi leo. Vitabu vilitafsiriwa kwa lugha mbalimbali hata kwa Kilatini na kwa njia hiyo Ibn Sina alikuwa pia mwalimu wa Ulaya katika tiba na falsafa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Avicenna, Encyclopaedia Britannica
  2. Von Dehsen, Christian D.; Scott L. Harris. Philosophers and Religious Leaders. Greenwood Press, p. 19. ISBN 1-5735-6152-5. 
  3. [1]
  4. [2]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikiquote-logo.svg
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu: