Encyclopedia Iranica
Encyclopædia Iranica ni kamusi elezo ya kitaalamu kuhusu historia, utamaduni, na ustaarabu wa watu wa Iran.
Ilianzishwa mwaka 1973 na profesa Ehsan Yarshater ikisimamishwa na taasisi ya Center for Iranian Studies kwenye Chuo Kikuu cha Columbia mjini New York.
Kamusi elezi hiyo inalenga kukusanya elimu ya kitaaluma kuhusu Iran wa leo lakini pia kuhusu maeneo yote yaliyokuwa sehemu za dunia ya Kiajemi katika historia. na uhusiano baina ya Uajemi na tamaduni nyingine kama vile China na Ulaya.[1] [2] Mradi unapanga kuchapisha jumla ya majuzuu 45 lakini tangu mwanzo maudhui yote inapatikana pia katika intaneti kupitia tovuti iranicaonline.org.
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- ↑ Boss (November 2003). Encyclopedia Iranica. Columbia College Today. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-10-18. Iliwekwa mnamo 2016-07-14.
- ↑ Trompf, Garry W. (2008). "Encyclopedia Iranica - 35: A New Agenda for Persian Studies?". Iran & the Caucasus 12 (2): 385–395. .
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
- Tovuti ya Encyclopædia Iranica (na Wakfu wa Encyclopædia Iranica) . Ufikiaji wa maandishi kamili kwa nakala nyingi kutoka Encyclopædia .
- Tovuti ya Encyclopædia Iranica (na Chuo Kikuu cha Columbia) .