Kituo cha Anga cha Kimataifa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka ISS)
Jump to navigation Jump to search
ISS mnamo mwaka 2010

Kituo cha Anga cha Kimataifa (kwa Kiingereza International Space Station, ISS) ni satelaiti inayozunguka Dunia katika kwenye umbali wa takriban kilomita 400. ISS ilianzishwa kutokana na mapatano baina ya mamlaka za usafiri wa angani za NASA (Marekani), Roskosmos (Urusi), ESA (Umoja wa Ulaya), Japani na Kanada.

Ujenzi wa kituo[hariri | hariri chanzo]

Kilianza kujengwa kwa kuunganisha sehemu zilizobebwa angani kwa roketi tangu Novemba 1998. Sehemu ya kwanza ilikuwa kitengo cha Kirusi chenye injini na nafasi ya kutunza fueli ikafuatwa na vitengo viwili kutoka Marekani na Urusi vyenye nafasi ya kukaliwa na wanaanga. Sehemu zilizofuata na kuunganishwa na kiini hiki zilibebwa kwa feri ya anga Space Shuttle ya Marekani na roketi za Kirusi. Tangu mwisho wa mradi wa Space Shuttle safari zote zinategemea roketi za Kirusi.

Tangu mwaka 2011 ukubwa wake ni mnamo mita 110 x 100 x 30. Kinazunguka Dunia kila baada ya dakika 92. Kuna mpango wa kuongeza kitengo cha Kirusi cha maabara katika mwaka 2019.

Tangu mwaka 2000 kinakaliwa na timu za wanaanga 2-3 wanaokaa kwa zamu za miezi kadhaa hadi kubadilishwa na kundi jipya. Mwanaanga mmoja huteuliwa kukaa kwa muda zaidi. Timu ya kwanza ya wanaanga (Warusi 2 na Mwamerika 1) ilifika mwaka 2000.

Mipango ya kuondoa kituo kwenye anga[hariri | hariri chanzo]

Kwa sasa imepangwa kutumia kituo hadi mwaka 2024. Imepangwa kuangusha kituo duniani kwa kulenga kwenye maeneo ya kusini ya Bahari ya Pasifiki. Kuna uwezekano kutumia vyombo vya anga vinavyosukuma kituo kuelekea panapotakiwa.

Shughuli kwenye ISS[hariri | hariri chanzo]

Kusudi kuu la kituo ni kuwa na maabara katika anga-nje. Katika mazingira yasiyo na graviti kuna nafasi ya kufanya majaribio mengi katika fani za biolojia, fizikia, kemia, tiba na astronomia. Kituo hiki kinabeba vifaa vinavyopima mnururisho wa mialimwengu (ing. cosmic rays) au mabadiliko ya nuru ya Jua.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]