Roskosmos

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Nembo ya Roskosmos

Roskosmos (rus. Роскосмос) ni jina la kifupi la shirika la serikali ya Urusi kwa shughuli za kiraia kwenye anga la nje. Jina kamili kwa Kirusi ni Государственная корпорация по космической деятельности (gosudarstvenaya korporatsiya po kosmocheskoi deyatelnosti "shirika ya kiserikali ya shughuli za angani").

Shirika hili lilianzishwa tarehe 1 Januari 2016 kwa amri ya rais Putin likachukua nafasi ya mamlaka ya kitaifa yenye jina lilelile.[1][2] kwa unganisha mamlaka ya awali na Shirika la Roketi na Anga la Nje (Объединенная ракетно-космическая корпорация, United Rocket and Space Corporation) iliyotengeneza vyombo vya anga.

Linahusika na miradi yote ya kiraia (tofauti na miradi ya kijeshi) ya Urusi. Makao makuu yapo Moscow na kituo cha kufunza wanaanga huko kwenye "Mji wa nyota" (Swjosdny Gorodok). Kituo cha kurusha roketi kinapatikana Baikonur katika Kazakhstan iliyokuwa kituo cha Umoja wa Kisovyeti.

Kwa jumla shirika la Roskosmos inachukua nafasi ya taasisi mbalimbali zilizohusika zamani ya ukomunisti katika Umoja wa Kisovyeti kupanga, kutengeneza na kutoa roketi na vyombo vya angani kama vile Sputnik 1, Soyuz na MIR.

Wanaanga Warusi (zamani za Umoja wa Kisovyeti)

Marejeo

  1. Russian space agency gets replaced by state corporation — Kremlin, TASS 2015-12-28, ikitazamiwa 2016-02-02
  2. Russian Space Follies, NASA Watch 2015-12-30, ikiangaliwa tar. 2016-02-02

Viungo vya Nje