Valentina Tereshkova
Mandhari
(Elekezwa kutoka Valentina Vladimirovna Tereshkova)
Valentina Vladimirovna Tereshkova (Kirusi Валентина Владимировна Терешкова) (* 6 Machi 1937) alikuwa mwanaanga kutoka Umoja wa Kisovieti na mwanamke wa kwanza aliyefika kwenye anga-nje.
Alikuwa mtoto wa mkulima aliyeendelea kusoma uhandisi akafaulu kupita mtihani kwa shule ya wanaanga mwaka 1962.
Tar. 16 Juni 1963 alirushwa kwa chombo cha angani Vostok 6 akazunguka dunia mara 49 akarudi duniani 19 Juni.