Herodia
Herodia (kwa Kigiriki Ηρωδιάς, Hērōdiás; (15 KK hivi — baada ya 39 BK) alikuwa mwanamke wa ukoo wa Herode huko Uyahudi chini ya himaya ya Dola la Roma.[1][2]
Ni maarufu hasa kwa kufanya mpango wa kumuua Yohane Mbatizaji hata akaufanikisha.
Uhusiano wa kifamilia
[hariri | hariri chanzo]- Baba yake alikuwa Aristobulo IV, mtoto wa Herode Mkuu.
- Mama yake alikuwa Berenike, aliyezaliwa na Kostabaro, gavana wa Idumea na Salome I, dada wa Herode Mkuu.
- Mume wake wa kwanza, Herode II, alikuwa pia mtoto wa Herode Mkuu na wa mke wake wa tatu, Mariamne II.
- Hatimaye aliolewa na Herode Antipa, mtoto mwingine wa Herode Mkuu ila kwa mke wa nne, Malthake.[3][4]
Herode Mkuu alipoua wanae Aleksanda na Aristobulo IV mwaka 7 KK, Herodia alibaki yatima, hivyo Herode alimuoza kwa mwanae Herode II.
Baadaye Herodia alitengana na mumewe ili aolewe na Herode Antipa, mtawala wa Galilaya na Perea.[5]
Herode II na Herodias walimzaa Salome (binti Herode).[6][7]
Kadiri ya Injili, Yohane Mbatizaji alifungwa na Herode Antipa kwa sababu ya kulaumu ndoa hiyo; hatimaye Herodia alifanya njama na binti yake Salome, akafaulu kumfanya Herode amkate kichwa Yohane.
Hatimaye Herode Antipa alinyang'anywa madaraka na kupelekwa uhamishoni sehemu za Ufaransa wa leo, ambako Herodia alimfuata.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Herodian Dynasty
- ↑ http://www.perseus.tufts.edu/hopper/text?doc=Perseus%3Atext%3A1999.01.0239%3Abook%3D16%3Achapter%3D2%3Asection%3D34
- ↑ Harold Hoehner, Herod Antipas: A Contemporary of Jesus Christ (Zondervan, 1983), page 132 - 134.
- ↑ see also, for example, E. Mary Smallwood, "Behind the New Testament", Greece & Rome, Second Series, Vol. 17, No. 1 (Apr., 1970), pp. 81-99
- ↑ According to the historian Josephus: Herodias took upon her to confound the laws of our country, and divorced herself from her husband while he was alive, and was married to Herod Antipas
- ↑ Taylor, V. (1966). The gospel according to St Mark, 2nd Edition. London: Macmillan (pp310ff.)
- ↑ As Josephus reports in Jewish Antiquities (Book XVIII, Chapter 5, 4):
Herodias, [...], was married to Herod, the son of Herod the Great by Mariamne II, the daughter of Simon the High Priest. [Herod II and Herodias] had a daughter, Salome...
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Gillman, Florence Morgan. Herodias: At Home in the Fox's Den. Interfaces. Collegeville, Minn.: Liturgical Press, 2003.
- Meier, John P. A Marginal Jew: Rethinking the Historical Jesus, Volume Two: Mentor, Message and Miracles. Anchor Bible Reference Library, New York: Doubleday, 1994.
- Theissen, Gerd. The Shadow of the Galilean: The Quest of the Historical Jesus in Narrative Form. Philadelphia: Fortress, 1987.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Herodias, A Dramatic Poem Archived 2012-12-10 at Archive.today by Joseph Converse Heywood.
- Herodias (third of the Three Tales) Archived 2012-12-16 at Archive.today, by Gustave Flaubert (English).
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Herodia kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |