Nenda kwa yaliyomo

Haki za binadamu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Haki za Kibinadamu)
Nembo ya Haki za binadamu

Kwa orodha za haki za binadamu angalia makala Tangazo kilimwengu la haki za binadamu

Haki za binadamu ni wazo la kuwa kila mtu anastahili haki kadhaa si kwa kutegemea cheo, wala taifa, wala tabaka, wala jinsia, wala dini kwa sababu tu yeye amezaliwa binadamu.

Haki hizi zimeorodheshwa hasa katika Azimio la Kimataifa juu ya Haki za Binadamu lililotolewa na Umoja wa Mataifa mwaka 1948. Tamko la UM lilikuwa kamilisho la majadiliano kuhusu haki hizi yaliyoendelea kwa karne kadhaa.

Hoja la kimsingi ni kwamba, "Watu wote wamezaliwa huru; hadhi na haki zao ni sawa. Wote wamejaliwa akili na dhamiri, hivyo yawapasa watendeane kindugu". (Kifungu 1 cha tangazo la 1948).

Mizizi ya haki hizo inapatikana katika falsafa na dini mbalimbali ya tangu kale, lakini ilikuwa wakati wa zama za mwangaza tangu karne ya 18 ya kwamba haki hizi zilijadiliwa kwa undani pamoja na swali: ni matokeo gani kuwepo kwa haki hizi yanaleta kwa utaratibu wa siasa, serikali na jamii.

Mfano wa haki za kimsingi

[hariri | hariri chanzo]

Haki za binadamu za kimsingi ni pamoja na:

  • Kuishi
  • Kuchagua kazi - kutokuwa mtumwa
  • Kuwa na mali
  • Kutoa maoni yake kwa uhuru
  • Kuwa salama, kutotishwa
  • Kuwa na kinga dhidi ya hatua za kisheria, pamoja na nafasi ya kupinga kwa njia halali
  • Kutokamatwa kwa kosa la mtu mwingine
  • Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya mahakama
  • Kutazamiwa kuwa bila ya hatia kabla mahakama haijatoa hukumu
  • Kuwa na uraia wa nchi fulani
  • Kupiga kura katika uchaguzi huru
  • Kupewa kimbilio kama nchi asilia inazuia uhuru wa msingi
  • Kuchagua dini na kuishi kufuatana na dini
  • Kupinga pamoja na wengine maazimio ya serikali kwa njia ya amani
  • Kupata elimu
  • Kufunga ndoa na mtu mzima yeyote

Kwa mengine angalia makala juu ya tangazo kilimwengu la haki za binadamu.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]

Shirika zinazopigania haki za binadamu

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Haki za binadamu kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.