Guruguru (nusufamilia)
Guruguru | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Guruguru koo-njano (Gerrhosaurus flavigularis)
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Jenasi 5, spishi 18:
|
Guruguru, kwa fasiri nyembamba, ni mijusi wa nusufamilia Gerrhosaurinae katika familia Gerrhosauridae. Spishi za nusufamilia nyingine, Zonosaurinae, zinaitwa guruguru-visiwa. Mijusi hawa wana magamba magumu mgongoni. Mbavuni wana kunyanzi la ngozi kwa urefu mzima wa mwili. Mkia wa spishi za jenasi Tetradactylus ni mrefu sana, zaidi ya mara mbili ya urefu wa mwili. Na miguu yao ni mifupi au haipo. Kwa sababu ya hiyo huitwa guruguru-nyoka.
Nusufamilia hii ina spishi kubwa kabisa za Afrika: hadi sm 75. Lakini spishi nyingi ni sm 30-45. Huishi kati ya mawe na miamba, katika vishimo, katika vichuguu au takataka ya majani na matawi. Chakula chao ni wadudu hasa, kama panzi, mchwa na sisimizi, lakini majongoo, tandu, konokono na mijusi wengine pia, na spishi nyingine hula matunda na maua pia.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Broadleysaurus major, Guruguru Magamba-shupavu (Rough-scaled plated lizard)
- Cordylosaurus subtessellatus, Guruguru Mdogo (Blue-black plated lizard)
- Gerrhosaurus auritus, Guruguru wa Kalahari (Kalahari plated lizard)
- Gerrhosaurus bulsi, Guruguru wa Laurent (Laurent's plated lizard)
- Gerrhosaurus flavigularis, Guruguru Koo-njano (Yellow-throated plated lizard)
- Gerrhosaurus multilineatus, Guruguru Magamba-miinuko (Keeled plated lizard)
- Gerrhosaurus nigrolineatus, Guruguru Mlia-mweusi (Black-lined plated lizard)
- Gerrhosaurus skoogi, Guruguru-jangwa (Desert plated lizard)
- Gerrhosaurus typicus, Guruguru wa Karuu (Namaqua plated lizard)
- Matobosaurus maltzahni, Guruguru Mkubwa Magharibi (Western giant plated lizard)
- Matobosaurus validus, Guruguru Mkubwa wa Kawaida (Common giant plated lizard)
- Tetradactylus africanus, Guruguru-nyoka Mashariki (Eastern long-tailed seps)
- Tetradactylus breyeri, Guruguru-nyoka wa Breyer (Breyer's long-tailed seps)
- Tetradactylus eastwoodae, Guruguru-nyoka wa Eastwood (Eastwood's long-tailed seps)
- Tetradactylus ellenbergeri, Guruguru-nyoka wa Ellenberger (Ellenberger's long-tailed seps)
- Tetradactylus seps, Guruguru-nyoka Vidole-vitano (Five-toed whip lizard)
- Tetradactylus tetradactylus, Guruguru-nyoka wa Rasi (Cape long-tailed seps)
- Tetradactylus udzungwensis, Guruguru-nyoka wa Udzungwa (Udzungwa long-tailed seps)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Gurugu magamba-shupavu
-
Guruguru mdogo
-
Guruguru mlia-mweusi
-
Guruguru mkubwa wa kawaida
-
Gurugu mkia-mrefu vidole-vitano
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Guruguru (nusufamilia) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |