Gumawesi
Mandhari
Gumawesi (kwa Kiingereza: basalt) ni mwamba wa mgando wenye rangi nyeusi-nyeusi.
Imetokana na lava kiowevu iliyotoka kwenye volkeno na kupoa haraka. Gumawesi ni mwamba mgumu unaoweza kudumu muda mrefu.
Mawe ya gumawesi hutumiwa katika ujenzi wa barabara ama katika tabaka la kokoto chini ya uso wa njia au kama vibapa vinavyofanya uso wa njia. Karibu na volkeno za zamani penye gumawesi tele hutumiwa pia kwa ujenzi wa nyumba na vijiji au miji katika mazingira hayo huwa na nyumba nyeusi.
Aina maalumu ya gumawesi huyeyushwa kiwandani kwa joto kali na kupata umbo la nyuzi zinazotumiwa kufuma mikeka ya kuzuia moto katika utengenezaji wa magari au eropleni. Ni nyuzi mbadala kwa asbesto bila kuwa hatari kwa afya.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Wikisource has the text of the 1911 Encyclopædia Britannica article Basalt. |
- Basalt Columns
- Basalt in Northern Ireland Archived 24 Februari 2021 at the Wayback Machine.
- Lava–water interface
- PetDB, the Petrological Database Archived 20 Agosti 2008 at the Wayback Machine.
- Petrology of Lunar Rocks and Mare Basalts
- Pillow lava USGS
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Gumawesi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |