Nenda kwa yaliyomo

Mwamba wa mgando

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jinsi gani miamba ya mgando huundwa
Lava inayotoka nje ya volkeno inapoa na kuganda kuwa mwamba wa mgando
Tufo ni mwamba laini ya mgando nje

Mwamba wa mgando (kwa Kiingereza: igneous rock) ni moja ya aina tatu kuu za miamba, pamoja na mwamba mashapo na mwamba metamofia.

Miamba ya mgando huundwa kutokana kwa kupoa kwa magma au lava, yaani mwamba moto katika hali ya kiowevu jinsi inavyopatikana katika koti la Dunia.

Miamba hii hutokea kwa namna mbili tofauti zinazosababisha pia tabia tofauti ya miamba yenyewe:

  • miamba ya mgando nje (miamba ya kivolkeno, miamba ya lava, ing. extrusive igneous rock) hutokea nje ya ganda la Dunia, wakati magma inapanda juu na kutoka kwenye uso wa Dunia kama lava. Inatoka pia kwenye tako la bahari pale ambako mabamba ya gandunia yanaachana ambako lava hupoa katika maji ya bahari. Lava inayotoka hupoa haraka na kuunda miamba ya mgando nje kama vile gumawesi.
Miamba hii huwa na fuwele ndogo tu, mingine hutokea hata bila fuwele kabisa, kama kioo cha kivolkeno. Kama lava ina gesi nyingi ndani yake, hiyo gesi inakimbia hewani na kuacha nafasi kama mashimo ya povu katika mwamba unaopoa. Kama lava inarushwa hewani kwa nguvu kubwa hutokea pia vipande vidogo sana kama majivu pamoja na vipande vya mwamba wa awali ulivunjikwa na mlipuko, na yale yote huanguka na kuunda aina ya mwamba ulio laini unaoitwa tufo.
  • miamba ya mgando ndani (miamba ya magma, miamba ya vilindi, ing. intrusive igneous rock) hutokea ndani ya ganda la Dunia, chini ya uso wa ardhi. Magma inaingia katika nafasi kati ya matabaka ya miamba iliyopo, na pale hupoa polepole. Mchakato wa kupoa polepole unaruhusu fuwele kukua ndani ya mwamba unaopoa. Itale ni mojawapo ya miamba ya mgando ndani.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwamba wa mgando kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.