Nenda kwa yaliyomo

Gazeti la Kijerumani la Afrika ya Mashariki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Toleo la kwanza la mwaka 1899, mjini Dar es Salaam (kwa herufi za kale za Kijerumani)
Nakala ya 7 Julai 1916, mjini Morogoro (Dar es Salaam ilivamiwa tayari na Waingereza)

Gazeti la Kijerumani la Afrika ya Mashariki (kwa Kijerumani: Deutsch-Ostafrikanische Zeitung - DOAZ) lilikuwa gazeti la kila wiki lililotolewa kwa lugha ya Kijerumani katika mji wa Dar es Salaam. Lilichapishwa kuanzia mwaka 1899 hadi 1916 kwa Wajerumani walioshi Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Mnamo mwaka 1902 lilikuwa na matoleo 1,000.

Gazeti hilo lilitetea hasa matakwa na maslahi ya walowezi wa Kijerumani. Hapo lilipinga mara kwa mara siasa ya serikali, hasa ya gavana Albrecht von Rechenberg, pale ambapo ilisita kuwapa kipaumbele, hasa katika suala la kuwalazimisha Waafrika wazalendo kukubali mikataba ya kazi kwenye mashamba ya walowezi kwa mishahara waliyopenda. Likapinga pia masharti ya kisheria yaliyobana matumizi ya mjeledi kama adhabu dhidi ya Waafrika.

Mengineyo ni kwamba lilitangaza mawazo ya kibaguzi dhidi ya Waafrika wazalendo waliotazamwa katika gazeti hili kama watu wasio binadamu kamili.

Kabla ya Dar es Salaam kuvamiwa na Waingereza gazeti lilihamia Morogoro mwezi wa Agosti 1915 ambako toleo la mwisho lilitokea katika mwezi wa Agosti 1916 uleule.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gazeti la Kijerumani la Afrika ya Mashariki kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.