Gaudioso wa Napoli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Gaudioso wa Napoli (jina kamili kwa Kilatini: Septimius Celius Gaudiosus; pia: Sanctus Gaudiosus Africanus, yaani Mtakatifu Gaudioso Mwafrika; alifariki 455) alikuwa askofu wa Abitine, karibu na Karthago, leo nchini Tunisia.

Mwaka 439 alikimbia Afrika Kaskazini wakati wa dhuluma za Genseriki, mfalme wa Wavandali, dhidi ya Wakatoliki akahamia Napoli pamoja na askofu wa Karthago, Quodvultdeus, na wengineo.

Inasadikika kwamba ndiye aliyeingiza huko kanuni ya Augustino wa Hippo.[1][2]

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 27 Oktoba[3].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.