Nenda kwa yaliyomo

Galdino wa Sala

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Masalia yake katika kanisa kuu la Milano.

Galdino wa Sala (1096 hivi [1]18 Aprili 1176) alikuwa kardinali tena askofu mkuu wa Milano, Italia Kaskazini, miaka 1166-1176.[2]

Kwa nguvu zote aliunga mkono juhudi za Papa Alexander III, za Milano na za miji mingine ya Lombardia, dhidi ya Antipapa Victor IV (11591164) aliyetegemezwa na kaisari Frederick I Barbarossa.

Alihamasisha matengenezo ya mji ulioharibiwa na vita vya kupigania mamlaka.

Anakumbukwa pia kwa ukarimu wake kwa mafukara na kwa waliofungwa kutokana na madeni.

Alifariki baada ya kutoa hotuba dhidi ya wazushi.

Papa Alexander III mwenyewe alimtangaza mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 18 Aprili[3].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/49900 states that he was born in 1096; other accounts place it at any time in the first few decades of the 12th century
  2. Miranda, Salvador. "GALDINO". The Cardinals of the Holy Roman Church. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-05. Iliwekwa mnamo 3 Januari 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.