Fransisko Antoni Fasani
Mandhari
Fransisko Antoni Fasani (Lucera, 6 Agosti 1681 - Lucera, 29 Novemba 1742) alikuwa padri wa utawa wa Ndugu Wadogo Wakonventuali kutoka Italia Kusini.
Msomi mkubwa, alipenda sana kuhubiri na kufanya toba, pamoja na kuhurumia fukara na wenye shida yoyote kwa kutoa daima bila kusita hata mavazi yake kuvika ombaomba na kuwapa wote msaada wake wa Kikristo [1].
Alitangazwa na Papa Pius XII kuwa mwenye heri tarehe 15 Aprili 1951, halafu tarehe 13 Aprili 1986 Papa Yohane Paulo II alimtangaza kuwa mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Saint Francesco Antonio Fasani Ilihifadhiwa 22 Juni 2009 kwenye Wayback Machine. Patron Saint Index
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |