France 24

France 24 ni mtandao wa kimataifa wa habari ulio nchini Ufaransa, ukitangaza kwa Kifaransa, Kiingereza, Kiarabu, na Kihispania. Unatoa habari za ulimwengu kwa mtazamo wa siasa, uchumi, utamaduni, na masuala ya kimataifa. Kituo hiki kinamilikiwa na serikali na kinalenga kuwasilisha mtazamo wa Ufaransa kuhusu matukio ya dunia, kikishindana na mitandao mingine kama BBC , Al jazeera. France 24 inapeperusha habari kupitia televisheni, majukwaa ya kidijitali, na mitandao ya kijamii, ikitoa taarifa za moja kwa moja, ripoti za kina, na uchambuzi wa wataalamu. Makao yake makuu yako Paris, na inafikia hadhira duniani kote kupitia setilaiti, kebo, na matangazo ya moja kwa moja mtandaoni.
Bajeti yake kwa mwaka ni takriban milioni € 80. Inapata fedha kutoka kwa serikali ya Ufaransa, na makao yake iko mjini Issy-les-Moulineaux,[1] karibu na mji mkuu wa Paris.
Hivi sasa inatangaza habari kwa Kiingereza, Kiarabu na Kifaransa, ingawa Rais Nicolas Sarkozy alipendekeza kuwa kituo hicho kitangaze kwa lugha ya Kifaransa pekee.[2]
France24 inatangazwa kwa stesheni tatu tofauti: ya Kiingereza, ya Kifaransa na ya Kiarabu kuanzia saa nane mchana hadi saa sita usiku (kulingana na masaa ya Paris).[3][4]
Vipindi vyake
[hariri | hariri chanzo]- The News
- In The Papers
- In The Weeklies
- Business
- The Business Interview
- Beyond Business
- The France 24 Interview
- Environment
- Face-Off
- The France 24 Debate
- Weather
- Health
- Fashion
- Culture
- World Generation
- Lessons For the Future
- Reporters
- Top Story
- Web News
- Sport
- Caring
- The Week In Africa
- The Week In Maghreb
- The Week In Asia
- The Week In Europe
- The Week In the Americas
- The Week In the Middle East
- The Week In France
- Markets
- Opinions
- Report
- Lifestyle
Wafanyakazi wakuu
[hariri | hariri chanzo]- Mwenyekiti: Alain de Pouzilhac
- Meneja wa habari: Albert Ripamonti
- Msimamizi jalada: Jean Lesieur
- Msimamizi wa nakala za Kiarabu: Nahida Nakad
- Msimamizi wa teknolojia: Frédéric Brochard
- Meneja wa wafanyikazi: Béatrice Le Fouest
- Meneja wa fedha: Frédéric Genea
- Mkuu wa sheria: Anne Kack
- Utangazaji: Patrice Begay
Upatikanaji na matumaini
[hariri | hariri chanzo]Inapatikana nchini Uropa, Afrika na Mashariki ya Kati kwa njia ya satelaiti. Tovuti yake ni france24.com
France 24 inalenga kushindana na stesheni kama CNN International, BBC World News, Deutsche Welle, na Al Jazeera English.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Contact Us." France 24. Retrieved on 29 Oktoba 2009.
- ↑ La chaîne France 24 dans l'incertitude Ilihifadhiwa 17 Januari 2008 kwenye Wayback Machine., Le Monde
- ↑ http://www.france24.com/
- ↑ Inside France 24