Nenda kwa yaliyomo

Flora Mbasha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Flora Mbasha (pia anajulikana kwa majina Flora H. Mayalah; alizaliwa katika Hospitali ya Hindu Mandhal Mwanza, 1 Juni 1983) ni mwimbaji na mwandishi wa nyimbo za Injili kutoka nchini Tanzania. Baba yake aliitwa Henry Joseph Mayala ambaye kwa sasa ni Marehemu na mama yake anaitwa Calorin Moses Kulola. [1]

Historia fupi

[hariri | hariri chanzo]

Flora Mbasha ni Msukuma wa wilaya ya Sengerema katika mkoa wa Mwanza.

Flora ni mtoto wa pili kuzaliwa katika familia ya watano ambao wanne ni wa kike (Dorcus, Suzan, Esther na Flora) na mmoja ni wa kiume (anaitwa Benjamin).

Pia amekulia katika maadili ya dini ya Kikristo, wakati huo baba yake akiwa Askofu mkuu wa kanisa la Evangelistic Assemblies of God. Babu yake na bibi yake ndio waliomlea wakishirikiana na mama yake.

Flora Mbasha alianza kuimba akiwa darasa la tatu wakati huo akienda na mama zake wadogo kwaya hadi alipokuwa na miaka kumi na tatu alipoanza kushiriki kuimba kwaya kanisani na kuimbisha baadhi ya nyimbo.[2]

Flora alifunga ndoa tarehe 22 Septemba 2002. Baada ya ndoa Flora na mume wake walianza kushirikiana kuimba nyimbo za Injili wakiwa katika Word Alive Band.

Mwaka 2003 mwezi juni walipata mtoto wao wa kwanza wa kike waliomuita Elizabeth. Na mnamo mwaka 2014 aliachana na aliyekuwa mume wake Emmanuel Mbasha na kuolewa na mfanyabiashara Mr Daudi Kusekwa 30 Aprili 2017 na kufanikiwa kupata watoto watatu

Carlobeth Daudi Kusekwa

Estherbeth Daudi Kusekwa

Marybeth Daudi Kusekwa

Nje ya muziki sasa anaaduka kubwa la Nguo za harusi lijulikanalo kama Madam Flora Bridal Na pia alibadili Jina lake baada ya kuolewa na sasa anajulikana kama Madam Flora

Album alizonazo

[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2004 Flora alirekodi albamu yake ya kwanza aliyoita Jipe Moyo iliyokuwa na nyimbo 10, ambazo zote walishirikiana na mume wake Emmanuel Mbasha. Ni: Jipe Moyo, Aliteseka, Maisha ya ndoa, Hakuna tatizo kuu, Ukimwi, Tunaye Bwana, Majaribu, Ahsante Yesu, Kila Jambo).[3]

Baadaye walifanikiwa kutoa album nyingine ya pili ilyojulikana kwa jina la Unifiche ambayo nayo ilikuwa na nyimbo 8: Tanzania, Unifiche, Faida gani, Twende kwa Yesu, Yatima Tuwasaidie, Kwa kupigwa Kwake, Alale kwa Amani, Tupendane).[4]

Flora pia ana album ya tatu inayojulikana kama Furaha Yako yenye nyimbo 12 ambazo ni: Furaha yako nini, Kaza mwendo, Siku hiyo, Bwana ni mchungaji wangu, Mambo yote Peupe, Bwana Yesu alipokuwa, Mwanafunzi mmoja, Maovu yenu.[5]. [6] Flora Mbasha album ya Kwanza inaitwa JIPE MOYO ambayo ina nyimbo kumi (10)

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-11-09. Iliwekwa mnamo 2018-11-17.
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-11-09. Iliwekwa mnamo 2018-11-17.
  3. https://www.google.com/search?q=jipe+moyo+flora+mbasha&rlz=1C1CHBF_enTZ813TZ813&oq=jipe&aqs=chrome.4.69i59j69i57j0l4.12040j0j7&sourceid=chrome&ie=UTF-8
  4. https://www.google.com/search?q=unifiche+flora+mbasha&rlz=1C1CHBF_enTZ813TZ813&oq=unifiche&aqs=chrome.2.69i57j0l3.10679j0j7&sourceid=chrome&ie=UTF-8
  5. https://www.qobuz.com/gb-en/album/furaha-yako-flora-mbasha/3614592056542
  6. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-11-09. Iliwekwa mnamo 2018-11-17.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Flora Mbasha kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.