Filoromus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Filoromus (alifariki Aleksandria, 311 hivi) alikuwa akida Mkristo wa Misri, ambaye, akikataa mashauri ya ndugu zake, alifia dini yake kwa kukatwa kichwa pamoja na askofu Fileas na wenzake 650 hivi wakati wa dhuluma ya makaisari Diokletian na Galerius[1].

Kati ya majina yao kuna maaskofu Pakomi, Theodori na Petro, halafu Fausto, Didius, Amoni, Hesiki na Viktorina[2].

Masimulizi ya kifodini chao yaliandikwa kwa Kigiriki miaka 15 baadaye na sehemu fulani imetufikia.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 4 Februari[3] au 26 Novemba.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.