Ferreol wa Uzes

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Ferreol wa Uzes (Narbonne, 5304 Januari 581) alikuwa askofu wa Uzès (553-581; labda wa Nîmes pia) nchini Ufaransa.

Alijitahidi kuvuta Wayahudi katika Ukristo, jambo lililomfanya afukuzwe na mfalme Childebert I mwaka 555 hadi 558[1].

Alianzisha monasteri wa Kibenedikto na kuipatia kanuni iliyotunzwa hadi leo.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu, sawa na dada yake, Tarsisia wa Rodez, mkaapweke.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 4 Januari[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Vita Ferreoli, apud Marcus Antonius Dominicy, Ausberti Familia Rediviva, published in Paris, 1648 (Jewish Encyclopedia)
  2. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ferreol wa Uzes kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.