Fausto wa Aleksandria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Fausto wa Aleksandria (alifariki 304 hivi) alikuwa shemasi wa mji huo tangu katikati ya karne ya 3 hadi mwanzo wa karne ya 4.

Wakati wa dhuluma ya kaisari Valerian alipelekwa uhamishoni Libya pamoja na askofu Dionisi na mashemasi wenzake Eusebi na Keremone.

Baada ya kurudi Misri hao mashemasi watatu waliishi bila makao maalumu.

Wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian alikatwa kichwa.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Novemba.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.