Nenda kwa yaliyomo

Wanyama wa nyumbani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Faida za mifugo)

Wanyama wa nyumbani (kwa Kiingereza "pets") hutunzwa kwa umakini mwingi haswa kwa jamii ya Wazungu. Wao hufanya wanyama hawa wawe kama marafiki zao ambao wanawalinda, kuwalisha na kuwaangalia vizuri. Si ajabu kuona mnyama kama mbwa au paka akipewa malazi mema, chakula kinacholiwa na wenye nyumba na hata kupelekwa hospitalini iwapo anaugua.

Haya yote ni mageni kwa jamii ya Waafrika, hata hivyo jambo hili linaendelea kukumbatiwa huku Waafrika wakiiga na kuanza kuwalinda wanyama wao kwa tunu na tamasha.

Shirika la kuwalinda wanyama huwa zinaangalia sana kwamba mnyama asiteswe lakini aangaliwe vizuri Ilihifadhiwa 9 Septemba 2017 kwenye Wayback Machine., apewe chakula kinachofaa, alazwe mahali pema palipo joto na pasipo unyevu, atibiwe iwapo ana ugonjwa wowote. Unapopatikana ukitesa mnyama, unaweza ukakuchukulia hatua kali ya kisheria, kutozwa faini, kupokonywa mnyama mwathiriwa au hata kufungwa jela kwa kosa hilo.

Jambo hili limewafanya watu wengi ambao walikuwa wanataka kuwatesa wanyama waogope na waanze kuwapa heshima inayofaa. Katika jamii nyingi, mbwa hathaminiwi. Yeye huonekana kana kwamba ni mnyama asiye na heshima zake hata kufikia kupigwa hadharani na watu au hata kuitwa mbwa koko asiye makao.

Kusafisha wanyama wa nyumbani

[hariri | hariri chanzo]

Usafi ni jambo muhimu sana kwa wanyama wa nyumbani. Iwapo mbwa ana uchafu, huenda akawa na magonjwa au hata akapatwa na kupe, kunguni au chawa wanaopenda kukaa mahali pachafu. Yafaa mwenye mbwa ajihami kwa kufuata kisomo cha kumsafisha mbwa wake.

Kutibiwa kwa wanyama wa nyumbani

[hariri | hariri chanzo]

Hata kabla ya kuugua, wanyama wa nyumbani hupelekwa kwa madaktari maalumu wa wanyama (vet doctor). Madaktari hao wana kisomo cha juu kuhusu afya ya wanyama. Wao huwaangalia wanyama hao iwapo wana jambo lolote la kiafya linalowakumba. Iwapo kunalo, watawatibu na kuwapa dawa za kufaa.

Lishe ya wanyama wa nyumbani

[hariri | hariri chanzo]

Wanaofuga wanyama hao huwa wakinunua lishe maalumu ambayo itawafaa wanyama hao na kuwafanya wenye nguvu na afya njema. Lishe ya wanyama wa nyumbani ni jambo ambalo limetiliwa mkazo sana hivi kwamba kuna kampuni ambazo zimejiunda kama za kutengeneza chakula cha wanyama wa nyumbani.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wanyama wa nyumbani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.