Eutisi wa Nursia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Eutisi wa Nursia (alizaliwa Norcia, Umbria, Italia, karne ya 5; alifariki huko kabla ya mwaka 540, labda 487 hivi) alikuwa mmonaki ambaye, baada ya kuishi upwekeni na Fiorenso wa Nursia, akiwaleta wengi kwa Mungu kwa ushauri wake, hatimaye alikubali kuwa abati wa monasteri karibu na mji huo, ila alimuomba mwenzake aendelee na ukaapweke[1].

Habari zake zimesimuliwa na Papa Gregori I katika kitabu cha Majadiliano, sura ya 15.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Mei[2][3].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/90580
  2. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
  3. Οἱ Ὅσιοι Εὐτύχιος καὶ Φλωρέντιος. 23 Μαΐου. ΜΕΓΑΣ ΣΥΝΑΞΑΡΙΣΤΗΣ.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.