Ethel de Keyser

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ethel de keyser
Amezaliwa 4 November
Africa kusini
Nchi Africa kusini
Kazi yake Mwanaharakati wakupinga ubaguzi wa rangi

Ethel de Keyser , OBE alizaliwa mnamo mwaka (4 Novemba, 1926 - 16 Julai, 2004) alikuwa mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi kutoka Afrika Kusini aliyeishi London, Uingereza.

Maisha ya Awali[hariri | hariri chanzo]

Ethel Tarshish alizaliwa mnamo mwaka 1926, kwa wazazi Wayahudi ambao walihamia Afrika Kusini mara tu baada ya kuzaliwa kwake. (Baadhi ya kumbukumbu ziliweka kuzaliwa kwake huko Vilnius, baadhi Afrika Kusini. ) [1] [2] Baba yake alikuwa na kiwanda cha nguo nchini Afrika Kusini. Alienda kusoma chuo kikuu huko Uingereza na kuwa raia wa Uingereza. Alirudi Afrika Kusini mnamo 1960 baada ya mauaji ya Sharpeville na kuzuiliwa kwa kaka yake Jack Tarshish. [1]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Alijihusisha na kazi yake ya kupinga ubaguzi wa rangi. Alikuwa njiani kurejea Uingereza mwaka 1963 wakati Jack alipokamatwa tena kama mwanachama wa African National Congress . Alikuwa Afrika Kusini kwa kesi hiyo lakini alifukuzwa nchini baadaye, na Jack alifungwa jela miaka kumi na miwili. Huko Uingereza, alifanya kazi kwa London Symphony Orchestra huku akijitolea katika harakati za kupambana na Ubaguzi wa Rangi (Anti-Apartheid Movement /AAM), hatimaye na kuwa katibu mkuu. [3] Aliongoza kampeni za kudumisha vikwazo vya silaha vya Waingereza dhidi ya Afrika Kusini, na kukataa kutambuliwa katika utawala wa Ian Smith huko Rhodesia . Alisaidia kuandaa SATIS (South Africa The Imprisoned Society), mkutano na mtandao kwa wale wanaofanya kazi ya kuachilia wafungwa wa kisiasa.

Alikua mkurugenzi wa Mfuko wa Ulinzi na Msaada wa Uingereza kwa watu wa Kusini mwa Afrika (Defence and Aid Fund for Southern Africa/BDAF) mwaka 1981, na kuanzisha (Canon Collins Educational Trust for Southern Africa) pia. [3] Antony Sher alisema alikuwa "mkuu wake wa kisiasa" wakati huu. [4]

Baada ya 1994, kazi yake ilihama kutoka kwa mtazamo wa kupinga ubaguzi wa rangi kwenda katika masuala ya afya na elimu nchini Afrika Kusini, pamoja na VVU/UKIMWI. [1] [3] Alitunukiwa OBE kwa kazi yake katika masuala ya haki za binadamu mwaka 2001. [5]

Maisha Binafsi[hariri | hariri chanzo]

Ethel Tarshish aliolewa na mwigizaji David de Keyser kwa miaka kumi (kutoka 1949 hadi 1959), na alikuwa na uhusiano wa muda mrefu na mwandishi George Lamming . [1] [3] [6]

Ethel de Keyser alifariki akiwa na umri wa miaka 77 mnamo 16 Julai 2004, baada ya mshtuko wa moyo. [1] Alikuwa akitarajia kutunukiwa shahada ya heshima katika Chuo Kikuu cha Western Cape mwezi Septemba. [3] Wadhamini wa Canon Collins Educational Trust walianzisha ufadhili wa masomo kwa jina lake kama ukumbusho. [7]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 Paul Trewhela, "Ethel de Keyser: London Anti-Apartheid Activist", The Independent (30 July 2004).
  2. "Ethel de Keyser; Anti-Apartheid Campaigner with a Flair for Outwitting Spies", The Times (29 July 2004).
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 Robert Hughes and Mike Terry, "Ethel de Keyser; Dedicated and Lifelong Campaigner in the Struggle Against Apartheid" The Guardian (20 July 2004).
  4. Antony Sher, "Trafalgar's New Nelson", The Guardian (6 May 2001).
  5. "The New Year's Honours", BBC News (30 December 2000).
  6. Denis Herbstein (11 March 2021). "The unrepeatable Ethel de Keyser". Canon Collins Educational & Legal Assistance Trust. Iliwekwa mnamo 18 January 2022.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  7. "The Ethel de Keyser Scholarships Fund", Canon Collins Educational Trust.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ethel de Keyser kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.