Nenda kwa yaliyomo

Erakla wa Aleksandria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu ya Mt. Erakla.

Erakla wa Aleksandria (alifariki Aleksandria, 247/248) alikuwa askofu wa mji huo wa Misri tangu mwaka 231 hadi kifo chake.

Kabla ya hapo aliingia Ukristo kwa kuvutwa na kaka yake Plutarko na kwa kuwa kama yeye mwanafunzi wa Origen, akawa mwalimu mwenzake; hatimaye alimpokea katika uongozi wa chuo cha Aleksandria.

Kutokana na sifa zake kubwa alichaguliwa kuwa askofu mkuu wa nchi[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 4 Desemba[2][3].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  • St. Heraclas (Theoclas), 13th Pope of Alexandria.
  • Meinardus, Otto F.A. (2002). Two Thousand Years of Coptic Christianity. American University in Cairo Press. ISBN 978-977-424-757-6.
  • Atiya, Aziz S. The Coptic Encyclopedia. New York: Macmillan Publishing Co., 1991. ISBN 0-02-897025-X

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.