Epipodi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Epipodi (alifariki Lyon, mji mkuu wa Gallia, leo nchini Ufaransa, 22 Aprili 178) alikuwa kijana Mkristo aliyekatwa kichwa katika dhuluma ya kaisari Marcus Aurelius dhidi ya Ukristo iliyosababisha mauaji makubwa katika mji huo[1].

Siku mbili baadaye rafiki yake mkuu, Aleksanda wa Lyon, aliyekamatwa pamoja naye, alisulubiwa kwa ajili ya imani.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini[2][3].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[4].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. http://santiebeati.org/dettaglio/50310
  2. Ruinart. Acta Martyrum, 1859 ed., p. 119
  3. Phillips, Fr Andrew. "Latin Saints of the Orthodox Patriarchate of Rome". orthodoxengland.org.uk. Iliwekwa mnamo 2017-03-01. 
  4. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.