Mdudu Mdomo-ndani
Mdudu mdomo-ndani | ||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mdudu mkia-fyatuo wa jenasi Isotoma
| ||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||
| ||||||||
Ngazi za chini | ||||||||
Nusungeli 3: |
Wadudu mdomo-ndani ni arithropodi wadogo walio na mnasaba na wadudu wa kweli. Ngeli hii ina oda tatu: wadudu mkia-fyatuo (Collembola), wadudu mikia-miwili (Diplura) na wadudu mkia-sahili (Protura). Kama wadudu wa kweli wadudu hawa wana miguu sita lakini hawana mabawa na vipande vya mdomo viko ndani ya mfuko maalum katika kichwa. Kila pingili ya vipapasio ina misuli (kwa wadudu wa kweli pingili mbili za kwanza tu zina misuli). Madume hawaweki shahawa yao katika jike lakini huiweka katika kibumba juu ya aina ya kikonyo (spermatofori) ambacho jike hukiingiza katika ufunguzi wa uzazi wake akikubali. Majike wana kiungo cha kutaga mayai. Spishi nyingi hazina macho, lakini kuna spishi za Collembola ambazo zina macho madogo yasiyo na zaidi ya omatidio nane.
Uainishaji
[hariri | hariri chanzo]Tangu mwaka 2005 wanasayansi wameanza kushuku usahihi wa ngeli hii. Malinganisho ya ADN yanadokeza kwamba Collembola (wadudu mkia-fyatuo), Diplura (wadudu mikia-miwili) na Protura (wadudu mkia-sahili) hawana mnasaba karibu. Wataalamu wanafikiri sasa kwamba kila kundi ni ngeli tofauti na kwa hivyo ngeli Entognatha imekwisha kukiriwa.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Spishi ya Collembola (Sminthurus viridis)
-
Spishi ya Diplura (Campodea staphylinus)
-
Spishi ya Protura (Acerentomon sp.)