Nenda kwa yaliyomo

Mdudu Mkia-sahili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Protura)
Mdudu mkia-sahili
Mdudu mkia-sahili (Acerentomon sp.)
Mdudu mkia-sahili (Acerentomon sp.)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye mwili wa pingili na miguu ya kuunga wasio na ugwe wa mgongo)
Nusufaila: Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
Ngeli: Entognatha (Hexapoda bila mabawa)
Nusungeli: Protura
Silvestri, 1907
Ngazi za chini

Oda na familia:

Wadudu mkia-sahili ni wadudu wadogo bila mabawa wa nusungeli Protura (ngeli kufuatana na wataalamu wengi) katika nusufaila Hexapoda wasio na serki (cerci). Wana kiwiliwili kilichorefuka chenye urefu wa chini ya mm 2. Hawana macho wala vipapasio na wanakosa hata pigmenti na kwa hivyo wana rangi ya nyeupe au hudhurungi. Hubeba jozi ya kwanza ya miguu juu na kuitumia kama vipapasio. Spishi kadhaa zina spirakulo (spiracle) na trakea (trachea), lakini spishi nyingi hubadilisha gesi kwa njia ya ueneaji. Wadudu hawa wanatokea katika ardhi, chini ya mawe na nyuma ya gome la miti. Wakifugwa hula matitiri waliokufa, kuvu-mizizi na unga wa uyoga na msituni hula yumkini kuvu na maada ya mimea iliyokufa.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mdudu Mkia-sahili kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Makala hii kuhusu "Mdudu Mkia-sahili" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili Protura kutoka lugha ya Kilatini. Neno (au maneno) la jaribio ni mdudu mkia-sahili.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.