Mdudu Mikia-miwili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Diplura)
Mdudu mikia-miwili
Mdudu mikia-miwili (Campodea staphylinus
Mdudu mikia-miwili (Campodea staphylinus
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye mwili wa pingili na miguu ya kuunga wasio na ugwe wa mgongo)
Nusufaila: Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
Ngeli: Entognatha (Hexapoda bila mabawa)
Nusungeli: Diplura
Börner, 1904
Ngazi za chini

Oda na familia:

Wadudu mikia-miwili ni wadudu wadogo bila mabawa wa nusungeli Diplura (ngeli kufuatana na wataalamu wengi) katika nusufaila Hexapoda walio na mikia miwili ambayo siyo mikia kweli lakini serki (cerci) ndefu. Wana kiwiliwili kilichorefuka chenye urefu wa mm 2-5 (spishi kadhaa za jenasi Japyx zinaweza kufika mm 50). Hawana macho lakini wana vipapasio vyenye pingili 10 au zaidi kama shanga. Kiwiliwili hakina pigmenti isipokuwa serki nyeusi katika spishi kadhaa. Fumbatio inabeba vilengelenge vinavyofyonza unyevu kutoko mazingira (kama collophore kwa wadudu mkia-fyatuo). Wadudu hawa wanatokea katika udongo mnyevu, majani yaliyoanguka ardhini na mboji, na hula arithropodi wadogo sana, kuvu na maada ya viumbehai.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu "Mdudu Mikia-miwili" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili Diplura kutoka lugha ya Kilatini. Neno (au maneno) la jaribio ni mdudu mikia-miwili.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.