Nenda kwa yaliyomo

Mdudu Mkia-fyatuo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Collembola)
Mdudu mkia-fyatuo
Mdudu mkia-fyatuo wa jenasi Isotoma
Mdudu mkia-fyatuo wa jenasi Isotoma
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye mwili wa pingili na miguu ya kuunga wasio na ugwe wa mgongo)
Nusufaila: Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
Ngeli: Entognatha (Hexapoda bila mabawa)
Nusungeli: Collembola
Lubbock, 1870
Ngazi za chini

Oda 4:

Wadudu mkia-fyatuo ni wadudu wadogo bila mabawa wa nusungeli Collembola (ngeli kufuatana na wataalamu wengi) katika nusufaila Hexapoda walio na mkia kama springi. Kwa kawaida wadudu hawa wana urefu wa chini ya mm 6. Wale wa Entomobryomorpha na Poduromorpha wana mwili uliorefuka, lakini wale wa Symphypleona na Neelipleona wana mwili wa mviringo. Fumbatio ina pingili sita au kasa. Ile ya kwanza inabeba kasiba dogo kwa upande wa tumbo (collophore) ambayo inafanya kazi katika kunywa maji. Mwishoni kwa fumbatio kuna kiambatisho kama mkia chenye umbo wa kiuma (furcula). Kiambatisho hiki kimekunjika chini ya tumbo zaidi ya muda na kushikilika kwa mvuto na muundo mdogo unaoitwa retinaculum. Kikifyatuliwa kinagonga didhi ya tabaka la chini na mdudu atupwa juu kwa nguvu mbali na mbuai au hatari nyingine. Wadudu hawa hula maada ya viumbehai na vijiumbe.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Makala hiyo kuhusu "Mdudu Mkia-fyatuo" inatumia jina ambalo halijakuwepo kwa lugha ya Kiswahili. Jina hili linapendekezwa kwa jina la mnyama huyu au wanyama hawa amba(ye)(o) ha(wa)na jina kwa sasa.

Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.
Kamusi za Kiswahili hazina jina kwa mnyama huyu au wanyama hawa.