Nenda kwa yaliyomo

Nyasi-bahari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Enhalus)
Nyasi-bahari
Nyasi-bahari majani-membamba (Halodule uninervis)
Nyasi-bahari majani-membamba (Halodule uninervis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Monocots (Mimea ambayo mche wao una jani moja)
Oda: Alismatales (Mimea kama mjimbi)
R.Br. ex Bercht. & J.Presl
Ngazi za chini

Familia 4

Nyasi-bahari ni mimea ya baharini ya familia 4 za oda Alismatales: Cymodoceaceae, Hydrocharitaceae, Posidoniaceae na Zosteraceae, inayofanana na nyasi za kweli (Poales: Poaceae).

Ekolojia

[hariri | hariri chanzo]
Matotovu madoa-meupe hupatikana mara nyingi katika maeneo ya nyasi-bahari.

Kama mimea yote ya autotrofiki, nyasi-bahari zinafanya usanidimwanga katika maeneo chini ya maji yanayopata nuru na hutokea zaidi katika maji ya kipwani yanayokingwa ambapo zimeangika kwenye sakafu za mchanga au matope. Takriban spishi zote zinapitia uchavuchaji chini ya maji ya bahari na kukamilisha mzunguko wa maisha yao chini ya maji.

Nyanja za nyasi-bahari zinaweza kuwa ama monospesifiki (yenye spishi moja) au zenye spishi zilizochanganywa. Katika maeneo ya wastani, kwa kawaida spishi moja au chache hutawala (kama vile nyasi-bahari majani-mikunga Zostera marina katika Atlantiki ya Kaskazini), lakini nyanja za kitropiki kwa kawaida ni anuwai zaidi, spishi 13 zikiwa zimeandikwa nchini Ufilipino.

Nyanja za nyasi-bahari ni mifumekolojia anuwai yenye kuzalisha, na zinaweza kuhifadhi mamia ya spishi zinazohusishwa kutoka kwa faila zote, kwa mfano samaki wachanga na wapevu, miani na viani ya kiepifiti na inayoishi huria, moluska, daa-manyoya na minyoo-kuru. Spishi chache zilizingatiwa awali kujilisha moja kwa moja kwenye majani ya nyasi-bahari (kwa sababu moja maudhui yao ya chini ya lishe), lakini ukaguzi wa sayansi na mbinu bora za kufanya kazi zimeonyesha kuwa kula kwa nyasi-bahari ni kiungo muhimu katika mfuatano wa ulishano, na kulisha mamia ya spishi zinazojumuisha kasa, nguva, samaki, mabata bukini, mabata-maji, chani na kaa. Spishi fulani za samaki ambazo zinatembelea au kujilisha kwa nyasi-bahari hulea wachanga wao kwenye kapa au miamba ya kupakana.

Spishi za Afrika ya Mashariki

[hariri | hariri chanzo]