Emily Ruete

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Emily Ruete

Emily Ruete katika mavazi ya kitamaduni kama Marikia wa Zanzibar
Amezaliwa 30 Agosti 1844
Zanzibar
Amekufa 29 Februari 1924
Jena, Ujerumani
Kazi yake Marikia wa Sayyida Salme Zanzibar na Oman

Emily Ruete (30 Agosti 184429 Februari 1924)[1] alizaliwa Zanzibar kama “Salama binti Said’’, pia aliitwa Sayyida Salme [2], Malkia wa Zanzibar na Oman. Alikuwa mtoto wa mwisho kati ya 36 kwenye familia ya Sayyid Said bin Sultan Al-Busaid, Sultani wa Zanzibar, Muscat na Oman. Pia ni mwandishi wa kitabu kiitwacho Memoirs of an Arabian Princess from Zanzibar.

Maisha yake Zanzibar[hariri | hariri chanzo]

Salama binti Said alizaliwa mnamo tarehe 30 Agosti 1844, mwana wa Sultan Said na Jilfidan, suria mwenye asili ya Circassia. Aliishi katika hekalu la Bet il Mtoni lililopo umbali wa kilomita nane kutoka baharini ukanda wa kusini mwa stone Town. (Hekalu hilo lilibomoka mnamo mwaka 1914). Amekuwa akizungumza lugha mbili ambazo ni Kiarabu na Kiswahili. Mnamo mwaka 1851 alihamia Bet il Watoro, katika nyumba ya kaka yake Majid bin Said wa Zanaibar, aliyewahi kuwa Sultani. Kaka yake alimfundisha jinsi ya kuendesha gari na kurenga shabaha. Mnamo mwaka 1853 alihamia Bet il Tani pamoja na kaka yake. Alijifunza kwa siri jinsi ya kuandika, ambapo taaluma haikuruhusiwa kwa mwanamke kipindi kile.

Pindi baba yake anafariki mnamo mwaka 1856 akiwa na umri wa miaka kumi na miwili hivyo kupewa urithi wake. Urithi huu ulijuisha mali kama mashamba, makazi pamoja na kiasi cha Paundi 5,429. Baada ya kifo cha baba yake, kaka yake Sayyid Thuwaini bin Said al-Said alikuwa Sultani wa Muscat na Oman, wakati kaka yake Majidi alikuwa Sultani wa Zanzibar.

Mnamo mwaka 1859 mama yake alifariki na Salme akapewa mashamba kama urithi wake. Mwaka huo huo kulizuka mgogoro kati ya kaka zake Majid na Barghash bin Said wa Zanzibar. Ingawa alimpenda kaka ya Majid, dada yake Khwala alienda upande wa Barghash. Kwa sababu aliweza kuandika, alikuwa secretary wa kikundi cha Barghash akiwa na miaka kumi na mitano. Kwa msaada wa meli za wamarekani Barghash alishindwa na utawalaa wake kuangushwa. Barghasha alipelekwa utumwani Bombay kwa miaka miwili ma Salme alikimbilia Kisimbani kwenye moja ya makazi yake.

Hatimaye Salme akarudi Stone Town na kujiunga na Majid. Hii ilimtengenezea chuki kati ya kaka yake Barghash na Khwala dada yake.

Emily akiwa na Mumewe pamoja na watoto wao wawili.

Kipindi anaishi Stone Town aliweza kufahamiana na jirani yake ambaye alikuwa mfanyabiashara wa Kijerumani, Rudolph Heinrich Ruete (Kuzaliwa 10 Machi 1839; Kufariki 6 Agosti 1870) na kupata ujauzito wake. Agosti 1866 ilionekana Dhahiri kuwa Salma anaujazito, ilibidi akimbilia kwenye manuwari sindikiza ya Uingereza H.M.S. Highflyer iliyoongozwa na Nahodha Thomas Malcolm Sabine Pasley R.N na kupewa ruhusa kuingia kwenye moja ya koloni la Uingereza liitwalo Aden. Huko alikuwa Mkristo na kuubatizwa kabla ya ndoa yake iliyofanyika tarehe 30 Mei 1867. Salma aljifungua mtoto wa kiume ,Heinrich, huko Aden Desemba 1866 na kufariki pindi akiwa katika safari ya kutokea Ufaransa kwenda Ujerumani katika majira ya joto mwaka 1867. Wawili hao walihamia Hamburg Ujerumani.[3]

Maisha yake Ulaya[hariri | hariri chanzo]

Familia ya Ruetes iliishi Hamburg, ambapo walipata mtoto wa kiume na wa kike wawili. Watoto hao waliitwa:

  • Antonia Thawke Ruete (24 Machi 1868–?), aliyemuoa Eugene Brandeis (1846–1919) mwaka 1898 na kupata watoto wakike wawili.
  • Rudolph Said-Ruete (13 Aprili 1869 – 1 Mei 1946). A mwandishi wa habari na vitabu, kwa kuanzishwa kwa kikundi cha Nazi Nazi Party, alijiuzuru uraia wake wa kijerumani mnamo mwaka 1934 na kwenda kuishi Marekani,huko kuimfanya awe raia wa Uingereza na kurafiki baada ya vita vya pili vya dunia huko Lucerne, Switzerland. Mnamo mwaka 1901, alimuoa Mary Therese Matthias (1872–?) na kupata mtoto moja wa kiume na mwingine wa kike, Werner Heinrich (1902-1962) na Salme Matilda Benvenuta Olga (1910–?). Kupitia ndoa hiyo, kulimfanya awe binamu wa Alfred Moritz, Baron Melchett wa kwanza, aliyekuwa mwenyekiti wa kwanza wa Imperial Chemical Industries.

Mume wake alifariki mnamo mwaka 1870 baada ya ajari mbaya ya treni ya umeme ya abiria, na kumwacha Ruete katika mazingira magumu ya kiuchumi baada ya mamlaka husika kukataa kumpatia urithi wake. Katika kupunnguza matatizo haya ya kiuchumi aliandika kitabu kinachoitwa Memoirs of an Arabian Princess from Zanzibar, kilichochapishwa kwa mara ya kwanza nchini Ujerumani mnamo mwaka 1886, na baadaye kuchapishwa Marekani na Ireland. Kitabu hicho kilitoa historia ya mwanamke wa Kiarabu kwa mara ya kwanza. Kitabu hicho kinampa msomaji picha ya maisha ya Zanzibar kati ya mwaka 1850 hadi 1865, pamoja na picha ya ndugu zake Majid bin Said wa Zanzibar na Barghash bin Said wa Zanzibar, Masultani wa kipindi kile Zanzibar.

Baada ya kifo cha mume wake, Emily Ruete alishikilliwa kutokana na mipango ya kikoloni ilifanya na Otto von Bismarck. Kulikuwa na tetesi kuwa Birsmarck alitaka kumfanya wanaye wa kiume kuwa moja ya Sultani wa Zanzibar. Emily alirudi Zanzibar mwaka 1885 na 1886, kitabu chake cha kumbukumbu kiitwacho, Memoirs of an Arabian Princess kilichapishwa nchini Ujerumani. [3] Kati yam waka 1889 and 1914, aliishi Beirut, Lebanon na Jaffa. Alifariki katika mji wa Jena huko Ujerumani, akiwa na umri wa miaka 79 kwa ugonjwa wa Nimonia

Mnamo mwaka 1992, kitabu cha An Arabian Princess Between Two Worlds kilichapishwa,huku akituma barua nyumbani kwao akiwaelezea maisha aliyoishi huko Ulaya, mwisho habari zake zilienea kwa umma wote.

Kuna maonyesho mbalimbali kuhusu Emily Ruete Jumba la makumbusho, Zanzibar iliyopo Stonetown, Jumba lililojengwa na kaka yake Sultan Barghash

Tetesi[hariri | hariri chanzo]

Emily Ruete amaonekana kama mhusika mdogo kwenye riwaya ya M.M. Kaye iitwayo Trade Wind. Kitabu hicho kilianzishwa mwishoni wa mwaka 1850 na kuonyesha uhusika wake na jaribio la kaka yake Barghash kukosa ufalme wa nduguye Majid, masilahi pamoja na ndoa yake na Rudolph

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]