Nenda kwa yaliyomo

Parachichi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Embe mafuta)
Mfano wa parachichi
Mfano wa Parachichi

Parachichi au embe mafuta (kwa Kiingereza avocado ) ni tunda lenye kokwa kubwa ndani na nyama ya kijani. Linatokana na mparachichi.

Asili ya tunda hili iko Amerika ya Kati na Wahispania walilipeleka kwa sehemu nyingine za Dunia. Tunda lina ngozi gumu kiasi yenye rangi ya kijani. Nyama ndani yake ni kibichi-njano hadi njano ya dhahabu Kama tunda linakatwa na nyama inaguswa na hewa rangi inabadilika baraja kutokana na kuoksidishwa. Hii inaweza kuzuiliwa kwa kupakia kidogo maji ya limau maana asidi ndani yake inazuia kuoksidishwa.

Matunda yanayopelekwa sokoni mara nyingi bado ni magumu lakini tunda linaiva hata baada ya kuvunwa. Baada ya kuonyesha ulaini tunda linaweza kuliwa. Pia parachichi hutumika kutengenezea juisi na ni miongoni mwa matunda yanayoongeza uwezo wa kufikiri na ni tajiri kwa vitamini.

Tunda huwa na kiwango kikubwa cha mafuta na hapa sababu linaitwa pia "embe mafuta". Uzito wa tunda moja unaweza kufikia hadi kilogramu 2, lakini kwa kawaida ni mnamo nusu kilo.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Parachichi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.