Elki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 23:12, 13 Aprili 2016 na 37.219.56.34 (majadiliano)
Elki
Elki (Alces alces)
Elki (Alces alces)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele)
Oda: Artiodactyla (Mamalia wanaokanyaga kwa kwato mbili-mbili)
Familia: Cervidae (Wanyama walio na mnasaba na kulungu)
Nusufamilia: Capreolinae (Wanyama wanaofanana na kulungu wa Dunia Mpya)
Jenasi: Alces
J.E. Gray, 1821
Spishi: A. alces
Linnaeus, 1758
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Elki (kutoka Kiing.: elk, Kisayansi: Alces alces) ni spishi kubwa inayoishi ya familia ya kulungu. Elki wanajulikana kwa vichwa vyao vikubwa na mashada yao ya pembe zinazogawanyika kama vidole vya kiganja; spishi nyingine za familia huwa na mashada ya pembe zinazogawanyika katika matawi. Kwa kawaida elki huishi misituni mwa kaskazini na misitu yenye miti ya kupukutika majani yake ya Nusudunia ya Kaskazini katika hali za nchi za wastani hadi maeneo ya chini ya Aktiki. Kutokana na uwindaji, elki wana makazi madogo zaidi. Sasa elki wengi wanapatikana Kanada, Alaska, Skandinavia na Urusi. Wao hula mimea ya ardhini na majini. Wanyama ambao huwinda elki ni mbwa-mwitu, dubu na binadamu. Tofauti na spishi zingine za kulungu, elki ni wanyama pweke na huwa hawaishi na kundi la elki wengine. Ingawa elki kwa kawaida hutembea polepole, wakasirishwapo elki waweza kuwa mkali na kusonga haraka. Wakati wa demani iliye majira yao ya kupandana, madume wa spishi hupigana na madume wengine na kumshindania jike.

Etimolojia na jina

Elki mwenye jina la kisayansi Alces alces hujulikana kama elk katika Uingereza na kama moose katika Amerika Kaskazini.

Jina la Kiingereza cha Kibritania linatoka lugha zingine za Kihindi-Kizungu, kwa mfano, elg kwa Kideni/Kinorwe, älg kwa Kiswidi, Elch kwa Kijerumani na łoś kwa Kipoli. Hata hivyo, katika Amerika Kaskazini neno la elk "elki" hutumika ili kurejelea mnyama tofauti, elki wa Kanada au pia huitwa wapiti (Cervus canadensis) ambaye ni mdogo zaidi na kisanaba tofauti na kulungu mwekundu wa Ulaya wa kati na magharibi.

Neno la moose kwanza liliingia Kiingereza mwaka wa 1606, na hutoka lugha za Kialgonkini (Kinarragansett moos na Kiabenaki cha Mashariki mos).

Elki dume aliyekua hurejelewa kama fahali, na elki jike ni dachia, na mtoto wa elki ni ndama.

Makazi na eneo

Amerika Kaskazini

Katika Amerika Kaskazini, elki huishi Kanada (mbali na Aktiki), Alaska, Uingereza Mpya, Milima yenye Miamba, Minesota, Peninsula ya Juu ya Michigan na Kijisiwa cha Kifalme cha Ziwa Kubwa. Katika eneo hili kubwa, kuna nususpishi zingi. Katika magharibi ya bara ya Amerika Kaskazini, idadi za elki zinafikia kaskazini mwa Kanada (Kolumbia ya Kibritania na Alberta) na spishi wengine wamepatikana milimani mwa Utah na Kolorado.

Ulaya

Katika Ulaya, elki wanapatikana katika Norwe, Uswidi, Ufini, Urusi, Polandi na nchi za Kibalti, na elki wachache katika Ucheki, Belarusi na Ukraini.