Elimu Mitaani.com
"Elimu Mitaani.com" | ||
---|---|---|
"Elimu Mitaani.com" kava | ||
Wimbo wa Dknob
kutoka katika albamu ya Elimu Mitaani.com | ||
Umetolewa | 2002-2003 | |
Umerekodiwa | 2002 | |
Aina ya wimbo | Hip hop | |
Urefu | 5:03 | |
Studio | Kokwa Records | |
Mtunzi | Dknob | |
Mtayarishaji | Miikka Mwamba |
"Elimu Mitaani.com" ni wimbo uliombwa na kutungwa na msanii wa hip hop kutoka nchini Tanzania, Dknob. Wimbo unatoka katika albamu yenye jina sawa na la wimbo. Wimbo ulitayarishwa na Miikka Mwamba kupitia studio za Kokwa Records. Wimbo ulitolewa kunako mwaka 2003.
Wimbo na mashairi
[hariri | hariri chanzo]Sehemu kubwa ya wimbo inahusu mahusiano ya Dknob na maisha ya mtaa jinsi baadhi ya watu wanavyomchukulia sivyo. Anasisitiza itolewe elimu ya mitaani, kwani, ni bora kushinda almasi. Kipande kingine anamsema: hata mitaani tulipozaliwa huwa wanasema tu, sema tu, na ndiyo maana anawaharibu dada zao na tuition wanatega. Hapa anamaanisha kwamba kuna watu wengine hupenda kuona wenzao wakishindwa katika majaribio yao ya maisha na yule aliyeharibiwa akigundua fulani ndiye aliyedanya, basi na yeye analipiza kisasi kwa namna yake (ndiyo maana anasema ninawaharibu dada zao na tuition wanatega). Menginye anasisitiza juu ya kuwasaidia watoto wa mitaani. Wimbo huu hunoenakana kama ndiyo nembo iliyotoa Dknob pangoni. Ijapokuwa kulikuwa na nyimbo zingine awali zilitoka kama vile Kibongo Stance, Usiniache, na nyingine nyingi tu.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu wimbo wa hip hop bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |