Juhudi za Msela
"Juhudi za Msela" | ||
---|---|---|
"Juhudi za Msela" kava | ||
Wimbo wa Dknob
kutoka katika albamu ya Bomoa Mipango | ||
Umetolewa | 2004-2005 | |
Umerekodiwa | 2005 | |
Aina ya wimbo | Hip hop | |
Urefu | 5:03 | |
Studio | Midman Records | |
Mtunzi | Dknob | |
Mtayarishaji | Jonas Kiwale | |
Bomoa Mipango orodha ya nyimbo | ||
|
"Juhudi za Msela" ni jina la wimbo ulioimbwa na kutungwa na msanii wa hip hop kutoka nchini Tanzania, Dknob. Wimbo unatoka katika albamu Bomoa Mipango. Wimbo ulitayarishwa na Jonas Kiwile kupitia studio za Midaman Records. Wimbo ulitolewa kunako mwaka 2005.
Wimbo na mashairi
[hariri | hariri chanzo]Katika mashari yake anaanza kwa kusema:
Mstari wa kwanza
Sitaki mbichi hizi, nataka mbivu mtini. Ndiyo maana saa yangu iko mbele dakika kumi. Karibu sana backstage yangu viwanjani, para kichwani, bandara shingoni, albamu sokoni - nnabuku mfukoni.
Halafu anaiitikia kwa kuimba:
Hizi ni juhudi za masela hakuna kulemba tunatafuta hela, Toka asubuhi mpaka night! Ngoja-ngoja kwanza na-fight!
Kijana niko vitani risasi zangu ni pini nachenguja na mashiti, lakini simwabudu shetani. Kukaba mtu kweupe na kivuli chake ndiyo zake...
Katika wimbo huu, hasa anamzingumzia maisha ya kija asiye na kazi halafu anajaribu kujitafutia kwa hali na mali. Hata kama itakuwa kwa kukaba au kuiba, basi ilimradi yeye mkono uende kinywani. Anazungumzia maisha ya vijana waliowengi mtaani.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu wimbo wa hip hop bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |