Nenda kwa yaliyomo

Kibongo Stance

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
"Kibongo Stance"
"Kibongo Stance" kava
Wimbo wa Dknob, P. One, na Villy
Umetolewa 2000-2001
Umerekodiwa 2000
Aina ya wimbo Hip hop
Urefu 6:10
Studio Kokwa Records
Mtunzi Watu tofauti
Mtayarishaji Miikka Mwamba

"Kibongo Stance" ni jina la wimbo ulioimbwa na kutungwa na mkusanyiko wa baadhi ya wasanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Tanzania, Kiwa Bizz. Wimbo hautoki katika albamu yoyote kwa vile ulikuwa wimbo wa ushirikiano wa wasanii wa Kiwalani kwa kipindi hicho. Hasa ilikuwa kama majibu kwa wasanii wenzao waliokuwa wakijiita "Kiwalani Gangsta Connection" au maarufu kama "KWGC". Wimbo ulileta mapinduzi makubwa na hisia kali kwa kwa kulinganisha nyimbo za awali zilizokuwa zikitolewa na wasanii wa Kiwalani. Baada ya hapo, mafanikio yakawa makubwa na kuleta hamasa kwa wasanii wengine kufanya nyimbo za maana kuliko hapo awali. Baadaye, wasanii hawa wakatengana kwa sababu ambazo si za msingi na hatimaye kila mtu kaenda kuwa msanii wa kujitegemea. Baadaye kukawa na makundi mengi baada ya kuona mkusanyiko huu, ikiwa ni pamoja na Miungu Watu Family, KG Connection, na mengineyo mengi.